Baada ya shutuma zinazoendelea mitandaoni kuhusu staa wa Ureno na klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo, kushangilia kwa mtindo ambao umekosolewa vikali na kupelekea mamlaka za soka Saudi Arabia kuanza kuchunguza kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kinyume na maadili, katika mchezo kati ya Al Nassr na Al Shabab. Jisajili na Meridianbet upate bonasi kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.
Shutuma hizo zimenikumbusha kipindi cha nyuma mwaka 2023 Septemba pale ambapo Ronaldo alipokumbwa na kashfa ya kumdhalilisha mwanamama ambaye ni shabiki yake kwa kumkumbatia kitu ambacho ni kinyume na sheria za nchi ya Iran kitu ambacho kwa sheria za nchi hiyo kosa hilo adhabu yake ni kuchapwa bakora 99, Nawakumbusha tu adhabu hiyo bado ipo pale pale endapo staa huyo ataingia kwenye nchi hiyo siku yeyote.
Je Ilikuaje Mpaka Ronaldo Kuhukumiwa Adhabu ya Viboko 99?
Ronaldo alikuwa nchini Iran kushiriki mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Asia wa Al-Nassr dhidi ya Persepolis mnamo Septemba 19. Kabla ya mechi, alipokelewa na mashabiki ambao walimwagia zawadi, ikiwa ni pamoja na jozi ya michoro ya kipekee iliyoandaliwa na mpiga picha Fatima Hamimi. Fatima, ambaye ana ulemavu anayechora kwa miguu yake, alimkabidhi Ronaldo aliyoichora yenye sura ya staa huyo kama ishara ya upendo kwa Ronaldo. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Katika wakati wa shukrani, Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 38 alimkumbatia mwanamke huyo na kumpa busu kichwani mwake. Ingawa ishara hiyo ilionekana kuwa ya kawaida kabisa, iriripotiwa kuzua utata nchini Iran. Ripoti kadhaa zinaashiria kuwa katika nchi hiyo, kugusa mwanamke mwingine wakati wa uhusiano unaweza kuchukuliwa kama uzinzi.
Ronaldo, ambaye amekuwa katika uhusiano wa muda mrefu na Georgina Rodriguez, sasa anajikuta kufungwa katika suala hilo gumu la kitamaduni.
Kulingana na vyombo vya habari vingi vya Iran, Ronaldo anadaiwa kuwa amehukumiwa kuchapwa viboko 99 kama adhabu kwa kitendo kile.
Walakini, serikali ya Iran ilikanusha madai hayo dhidi ya nyota huyo wa Ureno, na ilichapisha taarifa kwenye X.
“Tunakanusha kwa nguvu utoaji wa hukumu yoyote ya korti/mahakama dhidi ya mwanamichezo wa kimataifa yeyote nchini Iran. Ni jambo la kusikitisha kwamba uchapishaji wa habari hizo zisizo na msingi unaweza kuzidisha uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa vita dhidi ya taifa lililodhulumiwa la Palestina.
Inapaswa kueleweka kuwa Cristiano Ronaldo alisafiri kwenda Iran mnamo Septemba 18 na 19 kucheza mechi rasmi ya soka na alipokelewa vizuri sana na watu na mamlaka za nchi. Mkutano wake wa kweli na wa kibinadamu na Fatemeh Hamami pia ulisifiwa na kuheshimiwa na watu na mamlaka za michezo za nchi,” ilisomeka taarifa hiyo.