Magwiji wawili wa soka waliodumu kwenye ubora na ushindani kwa takribani miaka 15 Cristiano Ronaldo na Lionel Messi watakipiga nchini Saudia Arabia Mwezi wa pili mwakani.

Mchezo wa kirafiki baina ya Messi na Ronaldo unatarajiwa kupigwa nchini Saudia Arabia mwezi wa pili tarehe 24 mwaka 2024 katika mji mkuu nchini humo unaofahamika kama Riyadh.ronaldoMagwiji hao wameshakutana mara nyingi wakiwa katika vilabu tofauti barani ulaya, Lakini awamu hii wanakutana mmoja akiwa Marekani na mwingine akikipiga nchini Saudia Arabia.

Wakati Cristiano akiwa nchini Saudia na klabu ya Al Nassr walikutana katika mchezo wa kirafiki ambao ulivikutanisha vilabu vyao mwanzoni mwa mwaka huu Messi yeye akikipiga klabu ya PSG ya nchini Ufaransa kwa wakati huo.ronaldoMchezo huo unaelezwa unaweza kua wa mwisho kuwakutanisha magwiji hao ambao wamedumu kwenye ubora wao kwa muda mrefu zaidi, Kwani Ronaldo na Messi wote kwa pamoja wanaonekana hawana muda mrefu kwenye mpira wa miguu.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa