Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann inaelezwa hana mpango wa kutimka ndani ya klabu hiyo baada ya kuhusishwa na kujiunga na Man United.
Antoine Griezmann siku kadhaa nyuma amekua akihusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester United, Lakini vyanzo vya ndani kutoka klabu ya Atletico Madrid vinaeleza staa huyo hana mpango wa kutimka klabuni hapo.Inafahamika kua mshambuliaji huyo amewekeza akili yake ndani ya viunga vya Wanda Metropolitano baada ya kukataa ofa ya kujiunga klabu mbalimbali za Saudia, Hivo suala la yeye kujiunga na Man United ni jambo ambalo sio rahisi.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua kwenye kiwango kizuri sana msimu ndani ya Atletico Madrid, Jambo ambalo limewafanya klabu ya Manchester United kufukuzia saini ya mchezaji huyo.Antoine Griezmann ni wazi hana mpango wa kuondoka ndani ya klabu ya hiyo na kutimkia timu yeyote, Kwani kama ni kuondoka angeondoka dirisha kubwa lililopita ambapo alipewa ofa kubwa na vilabu kutoka nchini Saudia Arabia.