Staa wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Kai Havertz amefunguka kua anafurahia kuwepo ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake kaskazini mwa jiji la London.

Kai Havertz amesema anafurahia maisha ndani ya Arsenal kwasasa baada ya kjiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Chelsea kwenye dirisha kubwa la usajili lililopita.havertzKiungo huyo amekiri ilimuhitaji wiki kadhaa kupata imani ya mashabiki klabuni hapo kutokana na kua amejiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Chelsea ambao ni mahasimu wa Arsenal, Lakini ameeleza kwasasa kila kitu kipo sawa na anafurahia maisha kwa washika mitutu.

Kiungo huyo hajakua na mwanzo mzuri ndani ya klabu ya Arsenal na yeye mwenyewe amekiri hilo, Lakini ameweka wazi kucheza vizuri na kufunga magoli kutaweza kumuweka sawa.havertzKiungo Kai Havertz amekua mdomoni kwa mashabiki wengi wa soka mbali na wa klabu yake ya Arsenal kutokana na kutokuonesha ubora mkubwa kwenye timu hiyo mpaka sasa, Lakini mchezaji anaamini atafanya vizuri ndani ya timu hiyo ni suala la muda tu


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa