Timu ya taifa ya Italia maarufu kama Azzuri wako tayari kutetea ubingwa baada ya kufuzu michuano ya Euro mwaka 2024 ambayo inatarajiwa kupigwa nchini Ujerumani.

Italia jana walifanikiwa kupata sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Ukraine wakiwa ugenini ambapo iliwafanya kufikisha alama 14 na kukaa nafasi ya pili katika D na kujihakikishia kufuzu michuano hiyo.italiaAzzuri wameweza kufuzu kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa kwani walilingana alama na timu ya taifa ya Ukraine, Lakini wao walifanikiwa kufuzu wakiwa na magoli 7 huku wenzao Ukraine wakiwa na magoli 3.

Ikumbukwe kua Azzuri ndio walikua mabingwa wa michuano ya Euro 2020 baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Uingereza kwenye mikwaju ya penati, Sasa wamerudi tena kwajili ya kutetea ubingwa wao ambao walioutwaa mwaka 2020.italiaTimu ya taifa ya Italia kufuzu michuano ya Euro 2024 ni jambo kubwa kwa taifa hilo lenye historia kubwa kisoka ulimwenguni, Kwani miaka ya karibuni hiyo timu hiyo imekosa kushiriki michuano mikubwa wakiwa wameshindwa kufuzu kombe la dunia mara mbili mfululizo mwaka 2018, na 2022.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa