Paul Scholes amekiri kushangazwa na uwezo wa Casemiro kwenye mpira baada ya Mbrazil huyo kuonesha kiwango cha kuvutia la kiufundi kwa Manchester United kwenye Ligi ya Europa.

Scholes Ampigia "Salute" Casemiro

Casemiro, aliyesajiliwa kwa paundi milioni 70 majira ya joto kutoka Real Madrid, alitambulishwa wakati wa mapumziko kwa Scott McTominay huku United wakiandikisha ushindi mnono wa 2-0 dhidi ya Sheriff Tiraspol.

Scholes Ampigia "Salute" Casemiro

Akizungumza na BT Sport baada ya mchezo huo, Scholes alisema anaamini Casemiro ni mshindi baada ya kumtazama akicheza pamoja na mastaa wa ufundi Toni Kroos na Luka Modric kwa misimu kadhaa na alishangazwa na uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi, licha ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 kunyakua mataji kadhaa.

Scholes Ampigia "Salute" Casemiro

Alisema: ‘Alinishangaza kidogo kwa upigaji wake wa pasi za mbele”.

Licha ya ubora aliouonyesha, Scholes anaamini bado itachukua muda kwa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid kumwondoa McTominay na kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Erik ten Hag.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa