Rangnick: McTominay Ana Vitu vya Kinahodha

Kocha wa muda wa Manchester United, Ralf Rangnick amemwagia sifa kedekede mchezaji nyota wa Scotland Scott McTominay baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa FA Cup dhidi ya Aston Villa siku ya Jumatatu ambapo United iliibuka na ushindi wa 1-0.

McTominay alifunga bao pekee kwenye mchezo huo dakika ya 8 ya mchezo katika dimba la Old Trafford na amehusika kwenye mchango wa mabao mawili katika michezo mitatu iliyopita.

“Yeye ni kijana kutoka akademi, nguvu zake ni za ajabu,” Rangnick aliambia BBC Sport alipoulizwa kuhusu kiungo mfungaji wa United.

“Sasa pia anaanza kufunga mabao na pia kwa ujuzi fulani wa uongozi. Sitashangaa kama katika miaka kadhaa ijayo angekuwa nahodha wa timu hii.”

McTominay pia alikuwa amefanya jukumu lake katika ushindi wao wa awali, na kutoa bao la kwanza la kuvutia katika ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Burnley mwishoni mwa Desemba.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe