Shaw, Bissaka Bado wapo sana nje

Mabeki wa klabu ya Manchester United Luke Shaw na Aaron Wan Bissaka wanatarajiwa kuendelea kukaa nje ya uwanja kwa muda zaidi baada ya kupata majeraha.

Luke Shaw ambaye aliumia kabla ya Wan Bissaka anatarajiwa kurudia uwanjani mwezi Novemba baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, Huku ikikadiriwa na Wan Bissaka nae atakaa nje ya uwnaja kwa kipindi hichohicho.shawMabeki hao ndio wamekua mabeki chaguo la kwanza ndani ya Manchester United kwa upande wa kulia na kushoto, Hivo ni wazi kukosekana kwao kutaendelea kuigharimu timu hiyo katika michezo ijayo.

Beki Luke Shaw amekua kwenye kiwango bora sana chini ya kocha Erik Ten Hag jambo ambalo limemfanya aendelee kua chaguo la kwanza ndani ya timu hiyo lakini bahati mbaya ni kwasasa hataweza kuwepo uwanjani kuitumikia timu hiyo.shawWan Bissaka ambaye alikua akikaribia kutolewa kwa mkopo katika dirisha dogo lililopita mwezi Jnauari, Lakini alipambania nafasi ndani ya timu hiyo mpaka kua chaguo la kwanza la mwalimu ni wazi kukosekana kwake kwasasa ni pengo ndani ya Man United.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.