Wenyewe wanasema ukiwa nacho huwezi kuona thamani yake mpaka kiondoke na ndio kinachotokea kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United mpaka wakati huu ambapo wameanza kumkumbuka aliyekua golikipa wao David De Gea.
Mashabiki wa klabu hiyo kuna namna wanaamini David De Gea angewasaidia sana wakati huu ambao tayari wameharuhusu mabao 14 kwenye michuano yote mpaka sasa wakiwa na kipa Andre Onana.
Imekua mapema sana kwa mashabiki hao kumkumbuka golikipa huyo raia wa kimataifa wa Hispania, Kwani golikipa Andre Onana ndio kwanza ameanza msimu ndani ya timu hiyo japo wengi wanaamini De Gea anamzidi uwezo mbali golikipa huyo.
Mpaka sasa Manchester United imeshapoteza michezo minne katika michezo sita ambayo imecheza kwenye michuano yote msimu, Ikipoteza michezo mitatu kwenye ligi kuu ya Uingereza na mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya.
Golikipa Andre Onana jana aliruhusu goli la kizembe ambalo ndilo limefanya mashabiki wa Man United kuendelea kumnyooshea vidole na kuona sio mbadala sahihi wa raia wa kimataifa wa Hispania, Lakini ikumbukwe hata De Gea alianza vibaya katika siku zake za mwanzoni ndani ya Man United hivo mashabiki hao wanapaswa kua wavumilivu.

