Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Hotspurs Daniel Levy ameweka wazi kua ikitokea aliyekua mshambuliaji wao Harry Kane akarejea katika ligi kuu ya Uingereza siku moja basi wanaweza kumsaini tena.
Bosi huyo wa Tottenham amesema huwezi kujua yatakayotokea mbeleni lakini kama mshambuliaji huyo aterejea Uingereza siku moja na atataka kucheza ndani ya klabu hiyo basi watakua na uwezo wa kumsajili tena mchezaji huyo.
Klabu hiyo inaelezwa kua imeweka kipengele cha kumnunua tena mshambuliaji huyo kama atarejea kwenye ligi kuu ya Uingereza akiondoka ndani ya klabu ya Bayern Munich kwa miaka kadhaa ijayo.
Mshambuliaji Harry Kane aliondoka klabu hiyo ya Kaskazini mwa jiji la London baada ya kuitumikia kwa muda mrefu na kuvunja rekodi mbalimbali ikiwemo ya ufungaji bora wa muda wote ndani ya klabu hiyo.
Klabu ya Tottenham kupitia bosi Daniel Levy wamekua hawaweki kipengele cha kumnunua tena mchezaji waliyemuuza, Lakini kwa mshambuliaji Harry Kane wameweka na hii inakuonesha ni kwa kiasi gani mchezaji huyo anaheshimika klabuni hapo.

