Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, atasaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo.
Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta, 27, ataweza kuondoka Aston Villa miezi minane tu baada ya kujiunga na klabu hiyo.
Chelsea imekataa ofa ya Inter Milan kwa ajili ya kiungo wake aliyetwaa kombe la dunia N’Golo Kante, 29, ofa ambayo inajumuisha kubadilishana na kiungo wa Croatia Marcelo Brozovic, 27.

Mlinzi wa Manchester United Muingereza Chris Smalling, 30, hajahudhuria mazoezi wiki hii akikaribia kutua ligi ya Italia, Serie A, kwenye timu ya Roma, kwa uhamisho wa kudumu, timu ambayo aliichezea kwa mkopo msimu uliopita.
Kiungo wa Liverpool Georginio Wijnaldum, 29, amefanya mazungumzo yaliyoenda vizuri na meneja Jurgen Klopp kuhusu mustakabali wake klabuni hapo. Mholanzi huyo amebakiza mwaka mmoja kwenye kandarasi yake ya sasa pale Anfield.
Tetesi zinasema beki wa England na Tottenham Rose, 30, anakaribia kutimka Ligi kuu ya Uingereza kujiunga na kikosi cha Serie A Genoa.
Kipa wa Arsenal Muargentina Emiliano Martinez, 28, amekubali kandarasi ya miaka mine na Aston Villa, yenye thamani ya £60,000 kwa wiki, wakati huo vilabu hivyo vikitarajiwa kukubaliana ada ya uhamisho ya zaidi ya £15m.

Kiungo wa Manchester United na Brazil Fred, 27, amepuuza ripoti kwamba anaweza kuondoka msimu huu na kujiunga Galatasaray na Uturuki.
West Brom wako kwenye mazungumzo ya kumnasa mlinzi wa zamani wa Chelsea Branislav Ivanovic, 36, kwa uhamisho huru baada ya kutemwa na Zenit St Petersburg ya Urusi.
Kiungo wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, 27, yuko kwenye mazungumzo na klabu za Uholanzi za Vitesse Arnhem na Utrecht baada ya kutemwa na Sheffield United.
Mshambuliaji wa Liverpool na Wales Ben Woodburn, 20, anatarajiwa kujiunga na Sparta Rotterdam Uholanzi kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu mzima.

Tetesi zinasema ofa ya Newcastle ya £32m imekataliwa na Lille kwa ajili ya kumsaini kiungo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21, Boubakary Soumare.
Tetesi zinasema Fulham inataka kumsajili kiungo wa kireno, kutoka Benfica, Florentino Luis, 21, kwa mkopo wa muda mrefu kwa sharti la kumsajili moja kwa moja kwa ada ya £27m.
Porto imekataa ofa ya £22m kutoka Wolves kwa ajili ya kiungo wake Jesus Corona. Mkata wa nyota huyo wa Mexico mwenye miaka 27 una kipengele kinachotaka mpaka ilipwe ada ya £27m ndiyo aweze kuhama.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.
https://mrdn.co/c9mbiozafarasi


Latifa juma mohamed
New information.
Adelta
Asante kwa taarifa nzuri @meridianbettz
Johnmary joel
Kweli tetesi ziko vizuri na klabu pia zimejipanga kuwasajili wachezaji wazuri#meridianbett
Dorophina
Arsenal wamefanya Jambo zuri kumpa mkataba aubameyang yupo vizuri atawafaa katika msimu huu unaoanza
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa vizuri Kama Aubameyang Kama ataweka saini yake kwenye krabu hiyo ya Arsenal itakuwa vizuri
felister
Aubameyang ni mchezaji anayelipwa zaidi klabuni arsenal
Mwanahamisi
Asante kwa makala
Mwajumah
Arsenal wamefanya Jambo zuri kumpa mkataba aubameyang kwan ni mchezaji mzuri sana#Meridianbettz
Sauda
Klab zijipange kusajili vinara ambao wataleta mabadiliko katika timu
Fatina
Ni Jambo zuri kw arsenal kumpa shavu kijan
Caroline
Asante kwa taarifa
warda
Habari nzuri sana
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Ernest
Asante kwa habari nzuri za michezo , Hakika Meridianbet ni nyumba ya Burudani
Sadick
Timu za England zimejipanga vzr kufanya usajiri ambapo kuna uwezekano kutawala ligi ya mabingwa Ulaya#meridianbettz
Rose kapinga
Bonge la dili
rama
safii
Issa
Auba ameonyesha ukomavu ndan ya arsenal na kumemfanya the gunners imuamin zaid
Mariam mtandama
Vizur
Theckla
Habari njema
Sabrina
Arsenal wamefanya jambo jema kumpa mkataba Aubameyang
Furahav
Habari nzuri
Khadija
Safi sana#meridianbettz
lombo
vzur
Nasra
Safi sana
Devotha
Asante kwa makala
Shani
Usajili makini sana msimu huu
Frank P
Auba Arsenal wasitoe boko tu watafanya vizuri wakimuongezea mkataba
Gabriel
Tetesi hizi zimekaa vzur sana 👍
Theonestina
Asante meridianbet kwa taarifa
Saupha mohamed
Habari njema
Samira
Arsenal wamefanya jambo zuri sana kumbakisha Aubameyang
Shafii
Zimekaa poa.
Samiah
Safi
Amiri Kayera
Taalifa nzur za usajir
Magdalena
Arsenal wamefanya jambo la maana kumsajili Uyu kiungo
farida ahmadi
Habari njema Sana