Historia ya Soka Duniani

ULIANZIA WAPI HASA?

Kwa zaidi ya miaka 2000, Wachina wamekuwa wakicheza mpira wa cuju au zuqiu, ambao hutamkwa tsoo-joo unaohusu upigaji mpira shuti kwa kutumia mguu kwa Kiingereza “kickball”. Neno hilo hutumika kumaanisha kandanda hadi wa leo katika lugha hiyo….lakini ndio?

MCHANGO WA CHINA KWENYE SOKA

 

Mchezaji aliyevaa sare ya soka ya Cuju anavyoonekana katika makavazi ya soka ya Linzi ,Shandong, China.

Mchezaji aliyevaa sare ya soka ya Cuju anavyoonekana katika makumbusho ya soka ya Linzi ,Shandong, China.

Mchezo wa ‘Kickball’ ulivuma sana enzi za watawala wa Song, mwaka 960 hadi 1279. Mchezo huo wakati huo ulikuwa sehemu ya burudani mitaani.

Wajapani nao walikuwa na mchezo unaokaribiana na huo kwa jina Kemari, ambao ulianza kucheza miaka 500-600 baada ya Wachina na bado huchezwa leo. Wachezaji hukaa kwenye mduara na kupatiana mpira na kuhakikisha hauanguki chini.

Wagiriki ingawa kwa kuchelewa walikuwa na ‘Episkyros’ na Warumi ‘Harpastum’ ingawa miaka ya baadaye.

Mchezo kama huo wa China umezungumziwa katika kitabu maarufu cha The Splendours of the Eastern Capital (Ufarhari wa Jiji Kuu la Mashariki) kuhusu mji mkuu wa China wa wakati huo Kaifeng, mwaka 1120.

Kulingana na jinsi mchezo huo ulivyochezwa, wachezaji walihitajika kudumisha mpira hewani, yaani usitue. Kwa namna nyingine pia, mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa huku wachezaji wakihitajika kulenga goli. Kila timu pia ilikuwa na meneja, mkufunzi na nahodha.

Kulingana na Msomi wa Kijerumani Hans Ulrich Vogel, wahusika walikuwa ni watu kutoka familia tajiri, na pia wapiga shuti wa kitaalamu.

Cuju ulichezwa kama burudani kwenye sherehe rasmi kama zile za kuwalaki mabalozi.

Mchezo huo, ambao umegawanywa kwa ule wenye goli na lisilokuwa na goli, pia ulichewa kutumia sheria zake. Timu zilitumia sare zenye rangi tofauti, manahodha wakiwa na ishara za kuwatambua. Cha kustajaabisha ni kuwa walicheza bila walindalango. Wachezaji pia walihitaji kudumisha nidhamu ikiwemo kuwa na heshima.

Mshindi alikuwa mwenye mabao mengi na walitunukiwa kwa mvinyo na zawadi tofauti.

Kama tu mastaa wa soka ya sasa kama vile Messi na Ronaldo, wachezaji bora wa enzi hizo walipata umaarufu, kutajirika, na timu zao zilialikwa kwenye sherehe za kifalme. Pia walivutia ufuasi mkubwa kutoka kina dada. Katika mchuano mmoja, maelfu ya mashabiki wa kike waliojipamba kwa njia tofauti, walijitokeza kumtazama mchezaji nyota Li Guangyan ili kumvutia.

Nao pia walicheza jinsi ilivyonakiliwa na waandishi wa historia.

Wanawake waliruhusiwa kucheza?

Wanawake walikuwa pia wanashabikia mchezo huu. Shairi moja lwa karne ya 9 linakariria jinsi Li Guangyan, kansela wa wakati huo, alivyokuwa anacheza mpira huo.

“Alikuwa na kasi kama ya tumbili, uso wake kama wa kipanga, wanawake elfu tatu waliinamisha vichwa vyao kumtazama,” shairi hilo linasema.

Wanawake pia waliucheza. Mchoro mmoja unaonesha mwanamke akicheza ‘kickball’ kwenye bustani, nywele zake zikiwa zinavuma kwenye upepo, na mavazi yake kupepea.

Mwandishi mmoja wa habari za udaku kuhusu enzi ya Tang (mwaka 618-907) anaeleza kisa cha vijana watatu wa kike waliokuwa chini ya mti wanawatazama wanajeshi wakicheza karibu nao.. Mpira ulipotoka nje ya uwanja, mmoja wa wasichana hao “alinyoosha mguu wake kwa utulivu, akaudhibiti mpira kwa kidole chake cha gumba, na kisha akaupiga shuti kali na ukajipinda ukiwa hewani”.

 

Itaendelea..


SHINDA NA MERIDIANBET!

Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.

Cheza Sasa.

39 Komentara

    Mashabiki tunashukuru kwa makala @meridianbettz

    Jibu

    Kweli wachina wako vizuri meridianbett asanten kutupa taarifa za kimichezo huu mchezo sikuujua#meridianbett

    Jibu

    Asante kwa kutujuza maana wengine hatufahamu hiki kitu

    Jibu

    duh ndo kwanza nasikia Leo huu mchezo

    Jibu

    Asante kwa kutufahamisha

    Jibu

    Hasantee kwa makala Nzuri huu mchezo ndio kwanza nimehuona leo nilikuwa siujui

    Jibu

    Asante kwa makala#Meridianbettz

    Jibu

    Wachezaji wamejipanga vizuri sana

    Jibu

    Kumbe china mpira kitambo

    Jibu

    Mmmh hay mapya asanteh meridianbet kwa kutujuza maan ndo najua leo!

    Jibu

    Ila Mie naomna wachina bado Soka lao halipo juu sana#Meridianbettz

    Jibu

    Asnt kwa taarif

    Jibu

    Hii Makala Konki Konki Konki sanaaaa

    Jibu

    China wametisha sana,kumbe adi mpira wako vizur

    Jibu

    habari nzuri za historia ya soka

    Jibu

    Wachina wanajitahidi lkn soka halijawakubari

    Jibu

    ninachojua mimi ni waingeleza kuleta sheria ya jinsi kuucheza

    Jibu

    Soka ni mchezo wenye hamasa sana na inaongeza mahusiano

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    China wako vizuri Asante meridianbet kwa makala nzuri

    Jibu

    Noma sanaa.

    Jibu

    Da! Kumbe

    Jibu

    Hz ni habari nyingine tena ndio kwanza nazisikia

    Jibu

    wachina na mpira wapi na wapi#meridianbettz

    Jibu

    saf

    Jibu

    Dah noma

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

    Soka inaleta burudani na inaongeza mausiano bora kwa wanamichezo

    Jibu

    Imekaa poa sana 👍

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Asanteni kwa taarifa

    Jibu

    Hii makala nzuri tunashukuru kwa kutujuza mambo mazuri

    Jibu

    utafiti makini sana kuhusu mchezo wa mpira wa miguu#meridianbettz

    Jibu

    Habari nzurii

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Historia nzuri

    Jibu

    Ahsante kwa makala nzuri

    Jibu

    Historia imeekeweka sana

    Jibu

Acha ujumbe