Thierry Henry: Barcelona Haiwezi Kutwaa Ubingwa wa UCL

Mchezaji wa zamani wa Arsenal FC na mchambuzi wa soka, Thierry Henry, amehoji uwezo wa FC Barcelona kushindania ubingwa wa UEFA Champions League msimu huu, akieleza kuwa anaiona Bayern Munich pamoja na Arsenal FC wakiwa na nafasi kubwa zaidi ya kutwaa taji hilo.

Thierry Henry Barcelona Haiwezi Kutwaa Ubingwa wa UCL

Kauli ya Henry imekuja baada ya Barcelona kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na Newcastle United katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliochezwa kwenye Uwanja wa St James’ Park. Katika mchezo huo, Barcelona walinusurika kupoteza baada ya kupata penalti ya dakika za mwisho iliyofungwa na chipukizi wao Lamine Yamal na kuisawazishia timu hiyo bao muhimu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Thierry Henry Barcelona Haiwezi Kutwaa Ubingwa wa UCL

Wakati huo huo, Bayern Munich waliweka wazi ubora wao baada ya kuichapa Atalanta BC mabao 6-1 ugenini, licha ya mshambuliaji wao Harry Kane kuanza mchezo huo akiwa benchi kutokana na majeraha. Kwa upande wa Arsenal, timu hiyo imekuwa na msimu mzuri katika Champions League baada ya kushinda michezo yote nane ya hatua ya makundi, na sasa inajiandaa kukutana na Bayer Leverkusen katika hatua ya 16 bora.

Thierry Henry Barcelona Haiwezi Kutwaa Ubingwa wa UCL

Akizungumza na moja ya Chombo cha habari, Henry alisema Bayern Munich wanaonekana kuwa na uwiano mzuri zaidi kati ya ushambuliaji na ulinzi kuliko Barcelona, huku akibainisha kuwa Barca wakati mwingine hukosa uthabiti wa kiwango, jambo linalowafanya wasionekane kuwa tishio kubwa zaidi kwa sasa katika mbio za ubingwa wa Champions League.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.