Iran imetangaza kuwa haitashiriki mashindano ya Kombe la Dunia 2026 yatakayofanyika nchini Marekani ikiwa ni siku moja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kukutana na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, na kueleza kuwa Iran bado inakaribishwa kushiriki mashindano hayo.

Akizungumza na televisheni ya taifa ya Iran jana, Jumatano, Machi 11, 2026, Waziri wa Michezo wa Iran, Ahmad Donyamali amesema uamuzi huo umetokana na sababu za kisiasa na kiusalama na kubainisha kuwa hali ya sasa haiwaruhusu kushiriki mashindano hayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Kwa kuzingatia kuwa utawala hatuwezi kushiriki Kombe la Dunia kwa hali yoyote. Watoto wetu hawako salama na kimsingi mazingira ya kushiriki hayapo. Kutokana na vitendo viovu walivyofanya dhidi ya Iran, wametulazimisha vita viwili ndani ya miezi nane au tisa na kuua na kuwaua mashujaa maelfu ya watu wetu,” amesema.

Iran ambayo ipo kundi G la michuano ya Kombe la Dunia 2026 ilipangwa kucheza mechi zake za hatua ya makundi dhidi ya Ubelgiji, Misri na New Zealand katika miji ya Los Angeles na Seattle nchini Marekani.
Hata hivyo aliyekuwa Mkurugenzi wa Kanuni za Soka wa FIFA, James Kitching alisema: “Hakuna mfano wa kisasa wa hili na kwa mujibu wa kanuni za FIFA, wanayo mamlaka kamili kufanya maamuzi yoyote katika tukio la timu kujitoa. Hii ina maana kuwa, kwa mfano, timu inayojitoa haipaswi kubadilishwa na timu kutoka konfedresheni ile ile, au hata kubadilishwa kabisa. Je, mojawapo ya hali hizo inaweza kukubalika kisiasa ni swali tofauti.”

Kitching aliongeza kuwa kanuni za mashindano pia zinatoa adhabu za nidhamu kwa shirikisho lolote ambalo timu yake itajitoa. Hata hivyo, akizingatia hali ya mgogoro wa sasa, inaonekana FIFA haiwezi kutoa adhabu yoyote kwa Iran ikiwa watajitoa kutokana na sababu za kiasili zinazohusiana na vita.jambo ambalo linazingatiwa chini ya Kifungu cha Sita cha kanuni za Kombe la Dunia. Kifungu hicho kinasema kuwa
”FIFA inaweza kulichagua taifa lolote kuingia badala ya timu iliyotoka, huku ikitaja adhabu za kifedha kwa timu inayotoka”.

Iran ilistahiki kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuongoza Kundi A katika hatua ya tatu ya kualika Asia mwaka jana, na badala lake lina uwezekano mkubwa kuja kutoka bara la Asia, ingawa hilo haliko rahisi kama inavyotarajiwa. Kwa sasa, AFC na FIFA zinaendelea kufuatilia hali hii ili kuona ni taifa gani litaingizwa kama mbadala ikiwa Iran itajitoa.

