Marekani Kutumia “FIFA Pass” Kombe La Dunia 2026

Marekani imetangaza mfumo maalum wa viza kwa mashabiki watakaosafiri kwenda kushuhudia Kombe la Dunia la 2026. Mfumo huo mpya, unaojulikana kama “FIFA Pass”, umeanza kufanya kazi rasmi  wiki hii ukiwa na lengo la kuhakikisha mashabiki hawakumbani na matatizo ya kuingia nchini humo kipindi cha michuano.

Mashindano ya Kombe la Dunia yataandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico, huku Marekani ikibeba mzigo mkubwa wa mechi 78 kati ya 104. Michuano hiyo itaanza Juni 11 hadi Julai 19, na pazia litafungwa kwa fainali kali itakayochezwa katika Uwanja wa MetLife, New Jersey. Kwa ratiba hiyo nzito, maandalizi nje ya uwanja yamechukuliwa kwa uzito sana.

Marekani Kutumia “FIFA Pass” Kombe La Dunia 2026

Kupitia “FIFA Pass”, mashabiki kutoka mataifa yenye njia ngumu za maombi ya viza wanapewa nafasi ya kuharakishiwa, ili wasiikose michuano mikubwa duniani. Mpango huu ulitangazwa awali mwezi Novemba na aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, ukiwa kama pasi ya dharura kwa mashabiki wanaokimbizana na muda kabla ya mashindano kuanza.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hata hivyo, wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesisitiza kuwa kuwepo kwa FIFA Pass hakumaanishi ruhusa ya moja kwa moja ya kuingia nchini. Waombaji wote bado watalazimika kupitia ukaguzi mkali wa kiusalama na taratibu zote za uhamiaji, ili kuhakikisha usalama unabaki kipaumbele cha kwanza.

Marekani Kutumia “FIFA Pass” Kombe La Dunia 2026

Kwa mashabiki kutoka nchi zilizo kwenye mpango wa kuondolewa viza (Visa Waiver Program) kama Uingereza, mataifa mengi ya Ulaya, Japan na Australia, hawatalazimika kutumia mfumo huu mpya. Wataendelea kutumia mfumo wa ESTA kwa safari za hadi siku 90.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.