Baada ya Oliver Glasner kuthibitisha kuaga mwishoni mwa msimu, rada za Crystal Palace zinaonyesha jina moja la Andoni Iraola wa Bournemouth. Taarifa kutoka vyanzo vya karibu zinaeleza kuwa Palace wamepiga hatua kubwa kumtafuta meneja mpya na wapo mbioni kumtaja mrithi atakayechukua kijiti na kuendeleza kasi ya ushindani wa klabu hiyo.
Kuondoka kwa Glasner kunafunga ukurasa uliojaa matokeo na kumbukumbu nzuri. Kocha huyo raia wa Austria aliwapa Palace ladha ya taji kupitia FA Cup na Community Shield, akiacha alama ya kudumu kwenye historia ya klabu, ukirejesha hamasa ya mashabiki na kuifanya Palace kuwa timu ngumu kukabiliana nayo.
Hata hivyo, nyuma ya pazia kulikuwa na mvutano. Tofauti za kimtazamo kati ya Glasner na bodi kuhusu sera ya usajili na dira ya muda mrefu zilikua tatizo. Mwishowe, mafanikio uwanjani hayakuweza kufunika nyufa za uongozi, na maamuzi yakachukuliwa kwa maslahi ya mustakabali wa klabu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hapo ndipo Iraola anapoingia kwenye picha, kocha anayesifika kwa akili ya mchezo na falsafa ya kisasa. Akiwa Bournemouth, Mhispania huyo amejenga timu inayocheza soka la kasi, licha ya vikwazo vya bajeti. Hata kupoteza nyota muhimu kama Antoine Semenyo kwenda Manchester City hakukumvuruga, badala yake, aliendelea kuifanya Bournemouth kuwa moja ya timu zenye mbinu bora Ligi Kuu.
Kwa Palace, Iraola anaonekana kuwa chaguo sahihi, uwezo wake wa kuongoza timu, kukuza vipaji na kusoma mchezo kwa undani unawavutia wakubwa wa klabu. Ikiwa dili litakamilika, Selhurst Park inaweza kushuhudia enzi mpya.