UEFA Yatoa Burudani Kubwa Vigogo Wakichapana

Mashindano ya UEFA jana usiku yalileta burudani ya kiwango cha juu, yakishuhudia mabao, ushindani mkali na matokeo yaliyoacha gumzo barani Ulaya. Kuanzia mapambano ya vigogo wa soka hadi ushindi wa kushtukiza, mechi hizi zilithibitisha tena kwa nini UEFA hubaki kuwa michuano ya kipekee kwa mashabiki wa soka.

UEFA Yatoa Burudani Kubwa Vigogo Wakichapana

Huko Istanbul, Galatasaray na Atlético Madrid walitoshana nguvu kwa sare ya 1–1 katika mchezo uliotawaliwa na mbinu za kiufundi na presha ya hali ya juu. Qarabag FK waliendelea kung’ara barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa kishujaa wa mabao 3–2 dhidi ya Eintracht Frankfurt, wakionyesha uwezo mkubwa dhidi ya wababe hao wa Ujerumani. Bergamo nako kulishuhudia mtanange mkubwa, Athletic Club wakiibuka na ushindi wa 3–2 ugenini dhidi ya Atalanta katika mchezo uliojaa kasi.

UEFA Yatoa Burudani Kubwa Vigogo Wakichapana

Bayern Munich walithibitisha ubora wao kwa ushindi wa 2–0 dhidi ya Union St. Gilloise, wakitawala mchezo kwa umiliki wa mpira na ushambuliaji wa kasi. Stamford Bridge, Chelsea walipata ushindi mwembamba wa 1–0 dhidi ya Pafos FC, matokeo muhimu licha ya kutocheza katika kiwango chao bora. Jijini Turin, Juventus walionesha ukomavu kwa kuifunga Benfica 2–0 kwa mchezo uliosheheni uimara wa safu ya ulinzi na mashambulizi yenye ufanisi.

Bila kusahau, mbali na UEFA, meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

UEFA Yatoa Burudani Kubwa Vigogo Wakichapana

Liverpool hawakuwa na huruma nchini Ufaransa, wakiiadhibu Marseille kwa mabao 3–0 katika mchezo walioutumia kuonyesha ukubwa wao barani Ulaya. Newcastle United nao waliandika historia ya ushindi kwa kuichapa PSV Eindhoven 3–0, wakitawala mchezo kwa dakika zote 90.

UEFA Yatoa Burudani Kubwa Vigogo Wakichapana

Mabao yaliendelea kumiminika Prague ambako Barcelona waliibuka na ushindi wa kuvutia wa 4–2 dhidi ya Slavia Prague, wakionesha soka la kuvutia lakini pia wakiendelea kuacha maswali na wasiwasi juu ya safu yao ya ulinzi. 

UEFA Yatoa Burudani Kubwa Vigogo Wakichapana

Umebaki mzunguko mmoja kukamilisha hatua hii na kuelekea hatua ya 16 ya michuano hii ya UEFA na mpaka sasa kati ya timu nane zitakazofuzu moja kwa moja kwa hatua hiyo ni Arsenal na Bayern Munich pekee waliohakikisha tiketi yao ya kufuzu mpaka sasa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.