MSEMAJI wa Yanga Ali Kamwe amesema wao ndiyo wenye mashabiki bora Afrika na wengine waliobakia ni mbwembwe tu na hawana sifa ya kuwa mashabiki bora.
“Ukiona mtu anajadili mpira usiku wa manane ujue yamemfika hapa, sasa sisi Yanga SC hatuhitaji kufika huko.
“Sisi Yanga ndio tuna mashabiki bora Afrika na tunaenda kuionyesha Afrika kuwa walikosea kuwapa wale Simba.
“Sisi tunaenda kuijaza Benjamin Mkapa, maana vitu vyote wamejifunza kwetu sisi Yanga sasa wanakuwaje bora zaidi yetu.” Ali Kamwe.

