KOCHA mpya wa Simba Benchikha amesema kuwa ni muhimu kufanya kazi kwa ushirikiano kufikia malengo ya timu.
Hiyo huku akiweka wazi kuwa furaha yake kuwa katika timu hiyo ambayo ni kubwa Afrika.Kocha Benchikha ameweka wazi kuwa wanahitaji kufanya vizuri kufikia malengo ikiwa ni kutwaa ubingwa wa ligi ulio mikononi mwa Yanga.
Huku mpango wake ukitaka kuitengeneza timu hiyo ili iwe tishio Afrika na kutwaa mataji ambayo Simba wanatamani kuyapata.
“Nimekuja Simba kwa ajili ya kushinda, nimekuja Simba kubeba mataji, nimekuja Simba kwa ajili ya mashabiki wake.“Kikubwa ni kutengeneza timu bora yenye nguvu, hilo linawezekana kabisa kutokea kama tutakuwa kitu kimoja na kufanya kazi kwa moyo,” alisema.