Ligi kuu ya NBC ilirejea hapo jana ambapo michezo kadha wa kadha ilipigwa huku mchezo wa jioni kabisa ulikuwa ni ule uliowakutanisha kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Chamazi na Azam Fc waliichakaza Mtibwa kwa mabao 5-0 huku Kipre Junior akiingia kambani mara tatu, yani kiufupi alipiga hat-trick, huku Feisal akifunga bao moja na Lusajo Mwaikenda akifunga moja.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Baada ya ushindi huo Wanalamba lamba wanashika nafasi ya pili kwa kukusanya pointi zao 22 wakiwa na michezo yao 10 mpaka sasa huku Mtibwa wao wakiwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo.

Mtibwa wamepoteza mechi tatu mfululizo kwenye ligi wakikusanya alama zao tano kwenye mechi 10 ambazo wamecheza, wakiambulia ushindi mmoja pekee hadi sasa kwenye ligi.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Je kwa mwenendo huo ambao Mtibwa wanaendelea kuuonyesha kwenye ligi watashika nafasi ya ngapi mpaka ligi kumalizika?

