Batambuze Afungiwa Mechi Tatu

Beki wa  kushoto wa klabu ya Singida Big Stars Shafiq Batambuze amefungiwa michezo mitatu na faini ya shilingi laki tano baada ya kukiuka kanuni na taratibu zzilizowekwa na bodi ya ligi.

Mchezaji Shafiq Batambuze amefungiwa na kupigwa faini baada ya kuingia uwanjani kupasha misuli moto dakika kumi kabla ya muda wenyewe katika mchezo nambari 53 amabpo ulikutanisha vilabu vya Singida Big Stars na Simba.

Mchezaji huyo inaelezwa alipingana na maelekezo ya Kamishna na mratibu wa mchezo siku ambao walikuepo kusimamia mchezo huo siku hiyo na mchezaji huku mchezaji huyo akiwa uwanjani alionekana kumwaga vitu uwanjani kuashiria imani za kishirikina.

Vilevile bodi ya ligi baada ya kumfungia beki huyo vilevile imeshusha rungu kwa kocha msaidizi wa timu hiyo Mathias Lule na kocha wa magolikipa Steven Kiagundu ambao walikua wanamuamuru mchezaji huyo aendelee kubaki uwanjani hivo na wao watakosa michezo mitatu na faini ya milioni moja kila mmoja.

Ni wazi klabu ya Singida Big Stars itapata pengo baada ya Batambuze kufungiwa kwani amekua mhimili mkubwa kwa klabu hiyo kwenye safu ya ulinzi kutokana na ubora mkubwa ambao amekua akiuonesha.

Acha ujumbe