Beki wa Simba Lameck Lawi Apewa Ulinzi Mkubwa.

WAKATI MNYAMA SIMBA akiweka kambi katika mji wa Ismailia nchini Misri ikijiandaa na msim mpya bila kuwepo kwa mchezaji waliyemtambulisha Lameck Lawi. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

 

Kwani uko pande zipi? Popote ulipo taarifa ikufike nyota huyo wa Coastal Union yupo zake bize akipambana kukamilisha safari yake ya kwenda Ubelgiji.

 

Lameck Lawi Julai 8 alionekana akiingia na kutoka katika ubalozi wa Ubelgiji na alithibitisha kuwa ana mipango ya kwenda nchini humo.

 

Wakati Lameck Lawi akionekana ubalozini hapo, taarifa kutoka ndani ya Coastal Union zimefichuka kwamba beki huyo atauzwa nchini humo kwa moja ya klabu za huko.

 

TAJIRI mmoja ndani ya Coastal Union aliongeza Lameck Lawi akiuzwa Ubelgiji klabu yao itavuna fedha nyingi zaidi kushinda zile za Simba, Sh206 milioni ilizotaka kuzitumia kumnunua beki huyo.

 

“Coastal Union tayari tulishawarudishia fedha zao hao Simba, kama wanasema watafungua hiyo kesi shauri yao sisi tutamuuza beki wetu Ulaya, tutapata fedha nyingi zaidi,” alisema bosi huyo.

 

“Hapa kinachosubiriwa ni taratibu za safari yake kukamilika ili aondoke, tumeliangalia hili kwa upana mkubwa kwanza kwetu Coastal litatupa fedha nyingi, tutaisaidia Tanzania kama kijana kama huyu atakwenda huko lakini hata mchezaji atakwenda kunufaika zaidi.”

 

Simba ilitoa taarifa ya kukamilisha usajili wa beki huyo wa timu ya Taifa, Taifa Stars na kumtangaza kwenye mitandao ya kijamii, kabla ya viongozi wa Coastal kukanusha haijamuuza.

 

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

 

APEWA MLINZI WA KUTEMBEA NAE.

 

Yaani kwa sasa Lameck Lawi hatembei peke yake hapa mjini inadaiwa Coastal imempa mtu maalumu anayekwenda naye maeneo mbalimbali.

 

“Hao watu wa hizo klabu zenu kubwa (Simb, Yanga) hawaeleweki. Si mnamuona yuko na mtu. Yule ni mtu maalumu ambaye hatakiwi kuachana na Lawi hata kwa sekunde moja,” alisema bosi mmoja wa Wagosi.

 

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

Acha ujumbe