Jemedari Said Afunguka Ukweli Inshu ya Aziz Ki Yanga

Mchambuzi Nguli wa Soka nchini Jemedari Said Bi Kanzumari amesema kwamba Mburkina Faso Aziz Ki Yanga alishasajiliwa muda mrefu tu na Yanga, huku kukiwa na taarifa za mchezaji huyo kuhitajika na vilabu vingi vya Afrika ikiwemo CR Belouzidad ya Tunisia. Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Jemedari anasema kwamba “Tarehe 12 Juni Azizi Ki aliwekewa pesa za Kitanzania Tshs 520M kwenye benki moja hapa nchini na maelezo yake yalikuwa ni pesa ya usajili ambayo haikuanisha ni muda gani aidha mwaka mmoja au miaka miwili.”

“Pesa ambayo mhusika pia aliitoa baadae kwa matumizi yake mwenyewe kwenye siku hiyo hiyo.”

“Kinachoendelea mtandaoni ni jambo JEMA SANA kwenye Dunia ya mitandao ili kuleta mvuto na kutengeneza wasiwasi kwa wanayanga na baadae viongozi kuibuka “Mashujaa” kwa kushinda vita ya usajili. Lazima kutengeneza kufatiliwa kwenye social media platforms za klabu kwenye Dunia ya leo.”

“Mchezaji ambaye hajasajiliwa amekuja kufanya nini kiasi apewe na muda kwenye App ya klabu? Welcome Back King Ki, the world is all yours. Hongera viongozi kwa kumbakisha Top Scorer.

Rais wa Yanga, Mhandishi Hersi Said alisema hadi sasa kiungo wa klabu hiyo, Aziz Ki Yanga hajasaini mkataba mpya na kwamba mazungumzo yanaendelea na anaamini kwamba watafikia mwafaka.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Mhandisi Hersi aliyasema hayo akifanya mahojiano nchini Afrika Kusini ambapo amekiri kuwa kuna klabu nyingi zinataka kumsajili nyota huyo na kwamba itakuwa ni huzuni kwao kumpoteza raia huyo wa Burkina Faso kwani bado wanahitaji huduma yake.

“Mazungumzo yanaendelea, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kubaki [Yanga] lakini hatujafikia mwafaka,” amesema Hersi akiongeza kuwa Aziz Ki Yanga “anataka kubaki Yanga lakini mpira ni biashara siku hizi, hivyo anaweza akatamani kubaki lakini masuala ya kifedha yakamshawishi vinginevyo.”

Amesema kuwa alipomsajili Stephen Aziz Ki Yanga miaka miwili iliyopita alimweleza malengo yake ya kuiinua klabu hiyo, na kwamba nyota hiyo ni sehemu muhimu ya mageuzi ambayo yanaendelea ndani ya Jangwani.

Baada a haya yote kujitokeza, kwa upande wa mchezaji mwenyewe kishafika nchini alfajiri ya leo na atazungumza neno kwa mashabiki wa Yanga.

Wakati yote hayo yanaendelea waarabu wa Tunisia klabu ya CR Belouizdad inaelezwa wametuma ofa ya kumsajili mchezaji huyu ikiwa na dau la mshahara kwa mwaka dola 440,000/= sawa na Tsh Milion 93 kwa mwezi mmoja.

Pia wamemuahidi Gari la kifahari, sehemu nzuri ya kuishi “Apartment” na tiketi mbili za ndege kwa mwaka.

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

 

Acha ujumbe