Nahodha wa klabu ya Simba John Raphael Bocco amefanikiwa kuifungia klabu yake ya Simba mabao matatu kwenye ushindi wa goli nne kwa bila dhidi ya klabu ya Ruvu Shooting mcheo uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.
Klabu ya Simba imefanikiwa kufikisha alama 27 baada ya kucheza michezo 12 na hii ni baada ya kutoa kipigo kikali kwa maafande wa Ruvu cha mabao manne kwa bila huku Bocco akirudi kwenye ubora wake na kufunga mabao matatu.Simba walifanikiwa kuutawala mchezo kuanzia dakika ya kwanza mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa wekundu hao walikua wanaumiliki mchezo huo huku wenyeji wa mchezo huo wakitafuta mpira kwa tochi katika dimba la Benjamin Mkapa.
Kurudi kwa kiungo fundi wa klabu hiyo Claotus Chama imeendelea kuonesha umuhimu ake kwenye timu hiuyo baada ya kuifanya timu hiyo kucheza kwa utulivu na mipango mingi ikianzia kwake,Huku nahodha Bocco akitakata.Mabeki wa pembeni wa klabu hiyo Mohamed Hussein Zimbwe Jr na Shomari Kapombe ambae amefunga bao la tatu la mchezo pia wamekua kwenye kiwango bora sana huku wakiendeleza kile ambacho wameklua wakikifanya kwa miaka sasa.
Klabu ya Simba sasa imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 27 na kuwashusha watani zao Yanga wenye alama 26 huku Azam nao wakishuka hadi nafasi ya 3 na alama zao 26 huku wakiwa wamezidiwa tofauti ya magoli na Yanga.