Breaking News: Aziz Ki Bado Yupo Sana Yanga, Jiandaeni Kulia

Mashabiki wa Wapenzi wa Yanga waliokuwa roho juu, presha inapanda na kushuka sasa hali shwarii. Stephen Aziz Ki ametangaza kusalia klabuni hapo baada ya jitihada kubwa za kumbakisha kufanyka chini ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said. Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

 

Taarifa iliyotoka muda mfupi kutoka Yanga inaeleza kwamba mchezaji huyo ataendelea kusalia klabuni hapo, na hivyo zile habari zote zilizokuwa zinasambaa kuwa anaondoka ni rasmi zimekufa tena.

 

Awali kulikuwa na tetesi za Aziz Ki kuhitajika na vilabu vikubwa Afrika kama vile Kaizer Chiefs, Mamelod Sundwons, na CR Belouizdad lakini baada ya kauli ya Injinia Hersi ni kama alikoleza moto wa utammbulisho w Aziz Ki.

 

Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

 

Na baada ya kuwasili nchini mapema alfajiri ya leo, Aziz Ki aliongea na mashabiki wa Yanga kisha akawambia “Habari Wananchi bado niko hapa (Yanga)”

 

Mapema kabla ya habari hizi Meridianbet Sports tulisema kwamba Aziz Ki ataendelea kusalia Yanga kutoka na kauli tatu (3) kutoka kwa Rais wa klabu hiyo Injia Hersi Said, yeye mwenyewe mchezaji na Kiongozi mmoja aliyetaka jina lake kuhifadhiwa.

 

KAULI YA KWANZA ILIYOKAA KIMKAKATI.

“Ni mkakati wa klabu kuhakikisha mchezaji anabaki na majadiliano yanaendelea vizuri na hapana shaka tutarudi kufanya utambulisho ingawa kuna klabu nyingi zinamhitaji mchezaji.”

 

“Hivyo majadiliano yanaendelea na ninaweza kusema kuna nafasi kubwa kwa mchezaji kubakia lakini hatujakamilisha.

 

“Aliweka wazi kuwa anataka kubaki unajua nilimsaini miaka miwili iliyopita na nilimsajili kutoka Asec Mimosas na nikamueleza kuhusu ‘project’ yangu na nani nataka waipeleke klabu katika ngazi za juu na akawa sehemu muhimu ya program na mpango, ambao upo hi vyo majadiliano yakawa yaleyale na alisema wazi kuwa nahitaji kubaki hapa na kuipeleka Yanga katika ngazi ambazo unataka ifike.

 

“Lakini mpira ni biashara sasa unaweza kusema unataka kubaki lakini hali ya kifedha ikabadilisha mawazo kwa hiyo naweza kusema ni 60/40 (uwezekano wa kubaki),” alisema Hersi.

 

KAULI YA  AZIZ KI.

“Dube anakuja, (Joseph) Guede yupo, nisikilize, mimi ni kiungo, nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanakuwa wafungaji bora. Mimi ni kiungo kwa nini niwanie ufungaji bora, kwa nini ununue straika halafu utake kiungo awe mfungaji bora.

 

“Mimi ahadi yangu, nina matumaini straika wa Yanga atakuwa mfungaji bora msimu ujao Mungu akipenda, lakini sio Aziz, sahau kuhusu Aziz, mimi nitatoa asisti na siyo kuwa mfungaji bora,” alinukuliwa Aziz Ki katika moja ya mazungumzo yake.

 

KAULI YA KIONGOZI.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alisisitiza kuwa anahitaji kumkuta kiungo huyo kambini pindi atakapojiunga nayo na sio vinginevyo.

 

Kumekuwa na hisia kwamba uongozi wa Yanga umeshamalizana na mchezaji huyo na unachokifanya kwa sasa kutangaza kuwa hajasaini mkataba mpya ni kujaribu kutengeneza thamani ya tukio la utambulisho wa mkataba mpya wa mchezaji huyo.

 

Hisia hizo zinaweza kuthibitishwa na mmoja wa wajumbe katika uongozi wa Yanga ambaye hakupenda jina lake kutajwa ambaye alifichua kuwa Aziz Ki atakuwa kwenye kambi ya timu hiyo Afrika Kusini.

 

“Kambi ya maandalizi ya msimu mpya tutafanya Afrika Kusini na Aziz Ki atajiunga na timu huko hatuna wasiwasi wowote,” alisema kiongozi huyo.

 

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe