Aziz Ki Bado Yupoyupo Jangwani

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Stephane Aziz Ki raia wa kimataifa wa Burkinafaso amesalia ndani viunga vya Jangwani kwa mwaka mwingine tena baada ya tetesi nyingi kuibuka.

Aziz Ki ataendelea kuhudumu ndani ya klabu ya Yanga klabu hiyo ikiwa imethibitisha hilo mapema mchana wa leo, Taarifa ambayo ilikua inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa klabu hiyo kuona kama mchezaji wao bora wa klabu anasalia ndani ya klabu hiyo licha ya kuibuka kwa tetesi za yeye kutimka ndani ya timu hiyo.aziz kiKlabu ya Yanga inaonekana kudhamiria kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao kwani mpaka sasa wameonekana kujiimarisha zaidi, Ambapo wana wameweza kubakiza wachezaji wake bora klabuni lakini pia kuongeza wachezaji wengine ambao wataongeza ubora kikosini.

Kupitia Afisa habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe aliweka wazi kua mipango ya klabu hiyo msimu ujao ni kuhakikisha wanatwaa taji la Afrika, Hii inaendana na namna wanafanya sajili zao kwani sifa ya klabu yenye kuhitaji kufanya vizuri ni kubakiza wachezaji wako bora kikosini na kuongeza wachezaji wengine wenye ubora na ndicho ambacho wanakifanya Yanga.aziz kiKiungo Aziz Ki alihitajika na vilabu kadhaa kwaku Rais wa klabu hiyo Engineer Hersi Said alikiri kua ofa mbalimbali zimekuja klabuni hapo kumuhitaji mchezaji huyo, Lakini ni wazi klabu ya Yanga imefanya kazi kubwa kuhakikisha wanambakiza mchezaji huyo ndani ya viunga vya Jangwani kuelekea msimu ujao.

Acha ujumbe