Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema yeye anapendelea zaidi soka la kushambulia muda wote ndio maana amekuwa akishinda mabao mengi.
Na haijalishi nani anafunga maana mwanzo watu walikuwa wanalalamika kuwa eneo la ushambuliaji halifungi ila kwasasa kila mtu atakuwa anaona namna timu yake inavyofunga.
“Mimi napenda sana kucheza soka la kushambulia muda wote kama ambavyo nafanya kwasasa ndio maana nafunga mabao mengi.
“Watu wengi mwanzo walikuwa wanahofu na eneo langu la kushambulia ila sasa itakuwa wana majibu wameona yoyote anafunga lakini pia washambuliaji wangu Clement Mzize, Kennedy Musonda na Hafiz wote wanafunga na wanaenjoy,” alisema Gamondi.

