Kennedy Musonda ambaye kwasasa ni mali ya Yanga na anacheza katika nafasi ya ushambuliaji na, msimu wa 2017/2018 alifanikiwa kucheza mechi 15 na kupachika bao moja pekee katika timu ya Zanaco ambapo haikuwa ni kiwango kizuri.

Lakini Kennedy hakuishia tu hapo alicheza pia katika timu ya Green Eagles ya Zambia msimu wa 2019/20 pia na akacheza michezo 6 tu huku akifumania nyavu mara mbili. Lakini ukawa ni msimu ambao haukuwa mzuri kwake pia.
Msimu 2020/21 akasajiliwa na klabu ya Power Dynamos ambayo kwasasa ndiyo vinara wa ligi ya Zambia na akacheza jumla ya michezo 23 na kuingia kambani mara 4 tuu.

Msimu unaofuata wa 2021/22 mshambuliaji huyo alicheza mechi 24 na kufanikiwa kufu nga bao 3 pekee, huku ikiwa ni magoli machache sana kwa nafasi ambayo anacheza katika ligi.
Hakuishia hapao takwimu za mchezaji huyu za msimu unaofuata wa 2022/23 ziliimarika zaidi na kupanda ambapo sasa msimu huu amecheza michezo 17 na kupachika mabao 11 akiwa na Power Dynamos.

Na sasa Kennedy yupo katika ardhi ya Tanzania katika mitaa ya Twiga na Jangwani katika klabu ya Yanga ambapo anatarajiwa kuendeleza kiwango chake cha ufungaji. Je ataweza kuendeleza kufanya kile alichoishia kwenye timu aliyotoka? Muda utaongea.

