Sarabia Kutua Wolves

Mchezaji wa klabu ya PSG mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa Pablo Sarabia raia wa kimataifa wa Hispania Pablo Sarabia anakaribia kutua kwenye klabu ya Wolverhampton.

Kiungo Pablo Sarabia yuko mbioni kutimkia klabu ya Wolves ya nchini Uingereza baada ya kukosa nafasi kwa muda mrefu klabuni hapo, Hivo makubaliano yake na klabu ya PSG ni yeye kutimkia klabu nyingine ili aweze kupata nafasi ya kucheza zaidi.sarabiaKlabu ya Wolverhampton ipo tayari kukamilisha dili hilo kwa kiasi cha Euro milioni 5 baada ya kukubaliana na klabu ya PSG juu ya dau la kumchukia kiungo huyo. Dili hilo linaweza kukamilika ndani ya masaa machache yajayo baada ya pande zote mbili kukubaliana.

Pablo Sarabia atajiunga na klabu ya Wolverhampton siku za hivi karibuni kwani vilabu vimekubaliana pamoja na mchezaji huyo kukubali kujiunga na klabu hiyo, Mpaka sasa makubaliano ya kimaslahi na kusaini kandarasi ndio vimebaki kwa kiungo huyo.sarabiaKiungo huyo amehitajika na mwalimu na wa klabu ya Wolves Julien Lopetegui ambaye ameona raia mwenzake huyo wa Hispania anaweza kua mchezaji muhimu ndani ya klabu hiyo. Kiungo huyo sasa ataweza kupata nafasi ya kucheza ndani ya Wolves kwakua ni pendekezo la mwalimu ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe