Mchezo mwingine wa leo wa Ligi kuu ya NBC ni ule unaowakutanisha kati ya KMC dhidi ya Ruvu Shooting, huku kila timu ikihitaji kupata pointi 3 kujinasua kwenye nafasi ambayo yupo.

Wanakino Boys wametoka kupoteza mchezo wao walipokuwa nyumbani kwa mabao zaidi ya mawili huku nao Ruvu nao wakipoteza mbele ya vinara wa Ligi Yanga kwa bao 1 kwa sifuri.
KMC wapo nafasi ya 11 kwenye michezo 21 ambayo wamecheza hadi sasa, huku wakishinda mechi zao tano sare tano na kupoteza michezo nane hadi sasa wakiwa na alama 23.
Ruvu ya Mbwana Makata ndio vibonde wa ligi wakiwa na pointi 14 huku wakiwa hawakumbuki mechi ya mwisho wameshinda lini licha ya kuleta mwalimu mpya wa kukinoa kikosi hicho.

Timu zote zinahitaji ushindi. Nani kuibuka kidedea leo huku kila timu ikiwa na uhakika wa kupata matokeo mazuri. Tembelea Meridianbet ubashiri mechi hii.

