Jonathan Sowah yuko mbioni kjiunga na Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga akitokea klabu ya Al Nasr Benghaz ya Libya alipokuwa kwa mkopo, ambapo klabu yake ya awali ni Medeama. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Inaelezwa endapo dili lake litakamilika, kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kumuacha Joseph Guede aliyejiunga Januari mwaka huu akitokea Tuzlaspor FC ya Uturuki na kufunga mabao sita ya Ligi Kuu Bara. Lakini hata Kennedy Musonda na yeye huenda akapigwa chini muda wowote wiki ijayo.
Taarifa za ndani zinasema chanzo cha maamuzi ya mabosi hao ni kutoridhishwa na namba zao za ufungaji katika michezo waliyocheza msimu uliopita.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa.
Yanga imewahi kukutana na Sowah msimu uliopita kwenye mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama, mshambuliaji huyo akiwafunga Mabingwa hao kwa mikwaju wa penalti dakika ya 27, lakini Yanga walirudisha kupitia kiungo wao Pacome Zouzoua, mechi hiyo ikiisha kwa bao 1-1.
Sowah aliwasumbua sana Yanga kwenye mechi hiyo, hatua ambayo ikawafanya mabosi wa timu kuendelea kufuatilia zaidi ingawa baadaye wakapunguza kasi baada ya kusajiliwa na timu nyingine dirisha dogo.
Yanga imepata taarifa kwamba Sowah ameachana na klabu yake ya Al-Nasr Benghazi ya Libya ambayo ameitumikia kwa miezi sita tu.
Sowah, ameandika barua ya kutaka kuachana na klabu yake na sasa akikamilisha mchakato huo tu atakuja nchini haraka kumalizana na Mabingwa hao mara tatu mfululizo Ligi Kuu Bara.
Sowah mwenyewe amefunguka kuwa, amefuatwa na Yanga na wako kwenye hatua ya mwisho kumalizana akisema tangu alipokutana na klabu hiyo imebaki moyoni kwake.
“Bado tunaongea na viongozi wa Yanga, tunaelekea mwisho kabisa kuna mambo namalizana na klabu yangu, yakifikia mwisho nitakuja hapo Tanzania haraka, unajua tangu nilipokutana nao mashabiki wa timu hiyo wamebaki kwenye moyo wangu,”alisema Sowah.
Tangu ajiunge na Al-Nasr Benghazi dirisha dogo Sowah ameifungia mabao matano ambapo mchezo ambao aling’aa ni ule dhidi ya Al Hilal Benghaz aliofunga mabao manne peke yake wakati timu yake ikishinda kwa mabao 6-3.
Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.