KAGERA SUGAR WAANZA NA VIPONDO

FUNDO za walima miwa Kagera Sugar zinakatwa na wapinzani wao kila wanaposhuka uwanjani kwa kukwama kukomba pointi kwenye mechi mbili mfululizo za ligi ambazo ni dakika 180.

Kagera Sugar chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime kete yake ya kwanza ilikuwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma dhidi ya Mashujaa ilishuhudia ubao ukisoma Mashujaa 2-0 Kagera Sugar.kagera sugarMchezo huo ulichezwa Agosti 16 na mchezo wa pili Kagera Sugar ilipoteza dhidi ya Ihefu Agosti 19, Uwanja wa Highland Estate.

Mlinda mlango wa Kagera Sugar, Ramadhan Chalamanda amesema kuwa makosa ambayo walifanya kwenye mechi zilizopita watafanyia kazi ili urejea kwenye ubora.kagera sugar“Makosa ambayo tulifanya katika mechi zilizopita tunaamini benchi la ufundi limeona na litakuja na mbinu mpya zitakazotupa matokeo tutapambana wachezaji kupata matokeo chanya mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Acha ujumbe