KMC HAWAJAPOA KABISA MSIMU HUU

WAKUSANYA mapato wa Kinondoni KMC sio kinyonge ndani ya 2023 licha ya kuanza msimu kwa kuwa timu iliyotunguliwa mabao mengi ikiwa ugenini.

Ipo wazi kwamba mchezo wa kwanza kwa timu kufungwa mabao mengi ilikuwa ni ule uliowakutanisha Yanga 5-0 KMC mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.KMCInafunga 2023 ikiwa kwenye tano bora na mchezo wake uliopita ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma KMC 2-2 Simba.
Ipo nafasi ya nne kwenye msimamo na kwa upande wa utupiaji ni namba tano. Mkali wa kucheka na nyavu ni Wazir Junior akiwa katupia mabao 7 kibindoni.KMCMtambo wao wa mabao ni Awesu Awesu ana pasi nne za mabao. Kibindoni ina jumla ya pointi 21 baada ya kucheza mechi 14

Acha ujumbe