Kocha Dabo Aeleza Kilichowafelisha Kimataifa

YUSUPHU Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa wamegotea nafasi ya awali katika Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kushindwa kutumia nafasi.

Azam FC imeyaaga mashindano hayo kwa jumla ya penalti 3-4 baada ya matokeo ya jumla kuwa 3-3.daboMchezo wa kwanza ugenini ilishuhudia ubao ukisoma Bahir Dar 2-1 Azam FC katika mchezo wa pili Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam FC 2-1 Bahir Dar.

Licha ya mabao ya mapema ya Idd Suleiman na Prince Dube kufunga mabao ngoma ilikuwa ñzito kwa Azam FC .dabo“Tulikuwa na nafasi ya kupata matokeo bahati mbaya nafasi ambazo tumezitengeneza tumeshindwa kuzitumia imekuwa mbaya kwetu.
“Mwisho tumeona ni hatua ya penalti tumeondolewa hivyo ambacho tunakifanya ni kufanyia kazi makosa yetu,”.Alisema kocha Dabo

 

Acha ujumbe