Kocha Mpya wa Makipa Simba ana Mabalaa

RASMI Simba imetangaza kocha mpya wa makipa kwa ajili ya kuwa na timu hiyo kwa msimu wa 2023/24.

Ikumbukwe kwamba kocha huyo alikuwa ni shuhuda wa Yanga wakitwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2022/23 alipokuwa ndani ya Azam FC.simbaPia alishuhudia Azam FC ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa fainali wa Azam Sports Federation, Tanga ukiwa ni mchezo wake wa mwisho kuwa na uzi wa Azam FC.

Ni Daniel Cadena ambaye alikuwa akiwafundisha makocha wa Azam FC sasa atakuwa ndani ya kikosi cha Simba.simbaJulai 6 ametangazwa kocha huyo kuungana na timu hiyo ambayo inatarajia kuweka kambi Uturuki kwa maandalizi ya msimu mpya.

Cadena ameweka wazi kuwa ni furaha kwake kuwa na timu ya Simba na anaamini atafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.