Ofisa Habari wa Klabu ya Singida Fountain Gate Hussein Massanza amesema hakutakuwa na kiingilio katika mchezo wao wa kombe la shirikisho Barani Afrika dhidi ya Future ya nchini Misri.

Mchezo huo utapigwa tarehe 17, Jumapili katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, awali Singida waliwasafirisha mashabiki zao kutoka Singida hadi Dar na kurudi katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Kipanga ya Visiwani Zanzibar.

Sasa watafanya hivyo tena ili kutoa fursa kwa mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi ili kuwapa sapoti kwenye mchezo huo ambao wanahitaji zaidi ushindi kuliko chochote.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa