OKRAH AIBUKIWA BECHEM APEWA JEZI NAMBA 10

RASMI, Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Agustine Okrah amejiunga na klabu ya Bechem United ya Ghana, baada ya kuachana Kwa Makubaliano ya pande zote mbili na waliokuwa Waajiri wake Simba Mwanzoni mwa msimu huu,

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Moja ya jarida kubwa la Michezo la nchini Ghana, Jarida hilo limeripoti kuwa kiungo huyo ameingia makubaliano ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja tu na Waliokuwa Waajiri wake hao,OKRAHMara baada ya kutambulishwa Kwa mashabiki nyota huyo amekabidhiwa jezi namba 10 alivyokuwa akiivaa kabla hasajiliwa Simba.

“Okrah rasmi amerejea katika klabu yake ya zamani ya Bechem aliyokuwa anaichezea kabla ya kujiunga na Simba katika msimu uliopita,” ilisema taarifa hiyo.

Acha ujumbe