YANGA KUSHIRIKI AFRICAN FOOTBALL LEAGUE

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kuwa, Klabu ya Yanga itashiriki African Football League msimu ujao.

“Tulipitisha timu 24 lakini kutokana na ratiba kubana tukaona tuanze na timu 8 kwenye African Football League”yanga“Kwa mwaka huu tuna timu 8, lakini makubaliano ni timu 24, Ukanda wa CECAFA na COSAFA tunatakiwa kutoa timu 8, mwakani hata Yanga atakuwepo”

“Naamini timu zetu zitafanikiwa kuingia makundi katika mashindano ya kimataifa (CAF), na hayo ndiyo malengo yetu. Timu zinapocheza mashindano ya kimataifa tunaenda kama Tanzania, tukirudi kwenye ligi yetu kila mmoja apambane Kivyake,” alisema.

Acha ujumbe