Juventus Kumsajili Partey Kuziba Pengo la Pogba

Klabu ya Juventus inaelezwa iko kwenye mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ghana Thomas Partey kwajili ya kuziba pengo la kiungo Paul Pogba.

Kiungo Paul Pogba anashutumiwa na utumizi wa dawa za kuongeza nguvu mchezoni hivo Juventus wanataka kumsajili Partey kama Pogba atafungiwe kwajili ya kuchukua nafasi ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa.juventus parteyKiungo Paul Pogba alithibitika kua ametumia dawa za kuongeza nguvu mchezoni kutokana na vipimo vilivyochukuliwa tarehe 20 mwezi Agosti katika mchezo wa ligi kuu ya Italia dhidi ya klabu ya Udinese.

Mabingwa hao wa zamani wa soka nchini Italia wanaamini kama Pogba atafungiwa basi atafungiwa kwa muda mrefu hivo watahitaji mbadala wa kiungo huyo na Thomas Partey ndio anaonekana kama mbadala sahihi kwa klabu hiyo kuvaa viatu vya Pogba.juventus parteyKlabu ya Arsenal wanaonekana kua na hofu ya kumuachia Thomas Partey licha kumsajili kiungo Declan Rice, Lakini taarifa zinaeleza kama klabu ya Juventus itawasilisha ofa nzuri kwa Arsenal basi Washika mitutu hao kutoka jiji la London watakubali kumuachia kiungo huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.