Kikosi cha Klabu ya Simba kimekwea Alfajiri ya leo kueleka Botswana kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utakuwa ni wa pili kwao na itapigwa kesho Jumamosi saa 10 jioni.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas hivyo waligawana pointi mojamoja na langoni alikaa Ayoub Lakred ambaye yupo kwenye msafara.
Ukiachana na Mnyama huyo, meridianbet wanasema hivi cheza michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Aviator, poker, Roullette na mingine kibao ambayo inaweza kukupatia mkwanja wa maana. Cheza hapa.
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi chini ya Kocha Mkuu Abdelhak Benchika kina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Desemba 02, 2023 Botswana katika dakika 90 ambapo itakuwa ni kazi kwa wanaume 22 kusaka pointi tatu.
Simba imeondoka na wachezaji 20, benchi la ufundi katika msafara wake ukiambatana na viongozi wamewaacha baadhi ya wachezaji kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo John Bocco na Aishi Manula ambao ni majeruhi.
Wale waliopo kwenye msafara ni Henock Inonga, Mohamed Hussein, Fabrince Ngoma ambao ni miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo.