MATOLA ATOA YA MOYONI

Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola (Veron) ameweka wazi kuwa ligi inakwenda ukingoni jambo ambalo linaongeza nguvu kwa kila timu kupambana kupata matokeo.

Timu hiyo kwenye mechi tatu zilizopita ilipata ushindi katika mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Jamhuri.MATOLASimba leo, watakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kocha Matola amesema; “Kwa sasa ligi inakwenda ukingoni kila timu inapambana kupata matokeo mazuri ili kufikia malengo yake kwa kujiondoa kutoka nafasi ambayo ipo.

“Tunatambua ushindani ni mkubwa nasi tunafanya maandalizi mazuri kupata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza tupo tayari,”.Alisema MatolaMATOLAMchezo uliopita ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Simba 3-1 Singida Fountain Gate na kwenye mzunguko wa kwanza walipokutana na Mashujaa, Uwanja wa Lake Tanganyika ubao ulisoma Mashujaa 0-1 Simba bao lilifungwa na Saido Ntibanzokiza.

Acha ujumbe