Maxi Nzengeli Amtamani Mayele Yanga

KIUNGO wa Yanga, Maxi Mpia Nzengeli ameweka wazi kutamani kucheza na Fiston Mayele katika kikosi cha Yanga tofauti na alivyoondoka.

Maxi Nzengeli wakati anasajiliwa Yanga alimkuta mshambuliaji huyo akiwa kwenye hatua za mwisho za kujiunga na klabu ya Pyramid FC ya Misri.maxi nzengeliMaxi Nzengeli alisema kuwa alitamani kucheza na Mayele katika kikosi cha Yanga kwani anaamini angemfanya azidi kufunga mabao mengi huku akisema kuwa anamtakia kila la heri huko alipoenda.

“Nilitamani kucheza na Mayele ndani ya Yanga, wakati nafahamu kuwa naenda kujiunga na Yanga niliwaza kuwa nitaenda kucheza na Mayele na nitamsaidia kufanya vizuri zaidi.maxi nzengeli“Niliamini kuwa kwa ubora wangu na wake tungeifanya Yanga kuwa bora zaidi, mimi niseme tu nimtakie kila la heri alipoenda. Sisi kwa sasa tutaipambania Yanga ili izidi kuwa bora zaidi,” alisema mchezaji huyo.

Acha ujumbe