Mayele na Aziz Ki Kuikosa Azam Kesho

mayele-yanga

Mastaa wawili wa Yanga, Fiston Mayele na Stephane Aziz KI, wataukosa mchezo wa kesho wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.

Nyota hao walioipatia klabu ya Yanga ubingwa wa 29 wa Ligi Kuu Bara, watakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kuhusika kwenye majukumu ya timu zao za taifa zinazocheza michezo ya kufuzu AFCON.

Aziz Ki atacheza mchezo huo wa kufuzu AFCON akiwa na Burkina Faso itakayocheza na Cape Verde, huku Mayele anayeiwakilisha DR Congo atapambana na Gabon ambapo michezo yote hiyo itachezwa Juni 18. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

 

aziz ki

Mbali na kukosekana kwenye fainali ya FA, mastaa hao pia watakosekana katika usiku wa tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) zitakazofanyika Juni 12, 2023 Jijini Tanga baada ya kumalizika kwa fainali ya ASFC. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Kutokana na mastaa hao kukosekana kwenye tuzo hizo watachukuliwa hatua za kinidhamu endapo tu watakuwa hawajatoa taarifa kwenye mamlaka husika ikiwemo kupoteza nafasi ya ushindi, kufungiwa na kupigwa faini. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

Acha ujumbe