MIPANGO YA YANGA KIMATAIFA IPO HIVI

UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi kuwa, mipango yao mikubwa msimu huu katika michuano ya kimatafa inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ni kufika hatua ya makundi mara baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa zaidi ya miaka 20.

Yanga ambayo itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, inatarajiwa kuanza kuchanga karata zao rasmi Jumapili hii ya Agosti 20, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.YANGAKatika mchezo huo, Yanga inatarajiwa kucheza michezo yote miwili uwanjani hapo dhidi ya Asas Dijbout kutoka nchini Djibout kutokana na wapinzani wao kuomba kuutumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zao za nyumbani.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema kuelekea katika michuano ya kimataifa msimu huu ambapo wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, basi watapambana kuhakikisha wanatinga hatua ya makundi ambayo hawakufanikiwa kufika kwa muda mrefu.

“Yanga hatujafanikiwa kuchea makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa muda mrefu, hivyo msimu huu tunataka kuhakikisha tunafanikiwa kutinga katika makundi.YANGA“Watu wanaweza kusema msimu uliopita tulishiriki mpaka fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, iweje tuwaze makundi, nataka niwaambie kuwa kila jambo lina wakati wake na sasa kama tutafanikiwa kufika mbali zaidi ya hapa sawa lakini kwa sasa tunawaza zaidi kufikia hatua ya makundi,” alisema kiongozi huyo.

Acha ujumbe