Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema bado anaitengeneza timu yake ili kuhakikisha anakuwa na kikosi imara.
Aakizungumza mara ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa kumalizika na timu yake kuibuka na ushindi wa 4-2, Robertinho alisema, amejaribu kuwatumia wachezaji wake karibu wote ili aweze kuwaingiza mchezoni.“Nimewatumia kina Chama, Baleke, Luis, na wengine ili tutengeneze timu nzuri na namshukuru Mungu tumepata matokeo na nawapongeza wachezaji,” alisema kocha huyo raia wa kimataifa wa Brazil
Klabu ya Simba ilipata matokeo mazuri dhidi ya Mtibwa Sugar lakini mashabiki wa klabu hiyo walionekana kutokuridhishwa na kiwango cha timu hiyo, Lakini kocha Robertinho wa klabu hiyo ameendelea kusisitiza kua bado yuko kwenye mchakato wa kutengeneza timu hiyo.Kocha Robertinho amewatoa hofu mashabiki wa Simba ambao wamekua hawaridhidhwi na kiwango cha klabu hiyo, Kwani kocha huyo raia wa kimataifa wa Brazil bado anaijenga klabu hiyo.