Msuva Ahusishwa Kurejea Yanga

Mshambuliaji wa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Difaa El Jadida na Wydad Casablanca Simon Msuva anahusishwa kurejea klabu ya Yanga.

Yanga wameanza kuhusishwa na Msuva kwa kipindi kwa kirefu lakini tetesi hizi zimepamba moto kipindi hichi, Huku ikielezwa kuna mawasiliano baina ya kambi mbili yaani upande wa mchezaji lakini pia kwa upande wa mchezaji huyo.msuvaMshambuliaji huyo ambaye kwasasa yuko huru akiwa hana timu ya kuitumikia na hapo ndipo Yanga wamepata faida ya kutuma ofa kwa mchezaji huyo wakijaribu kumrudisha katika klabu hiyo ambayo aliitumikia kwa mafanikio.

Mshambuliaji Simon Msuva ni mmoja ya wachezaji ambao wamewahi kuitumikia klabu ya Yanga kwa mafanikio makubwa, Lakini pia kwa upande wake akifanya vizuri ambapo aliwahi kushinda kiatu cha mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania.msuvaTaarifa mpaka sasa zinaeleza kama mawasiliano yataenda sawasawa basi mshambuliaji huyo wa zamani wa Wydad Casablanca ya pale Morocco anaweza kuvaa jezi za Njano na kijani msimu huu katika michuano mbalimbali ambayo Yanga watakua wanashiriki.

Acha ujumbe