STAA wa Tanzania Simon Msuva amesema kuwa beki mpya wa Yanga Nickson Kibabage atawashangaza watu kwa kuwa ana uwezo mkubwa sana
Simon Msuva alisema hayo baada ya beki huyo kuungana na Yanga: ” Mimi nimecheza Yanga naijua Yanga ingawa siijui kwasasa kama ambavyo wakati nacheza pale, ila naamini ubora wa Kibabage kwa juhudi zake watu watashangaa,”
” Yanga ni timu kubwa, anatakiwa akienda pale atambue kwamba atawakuta wenzake ambao nao ni bora, kitakachomsaidia ni juhudi zake hasa mazoezini, anatakiwa sasa kufanya mazoezi mara mbili ya kile alichokuwa anafanya Singida, ”
” Mimi huwa nafanya naye sana mazoezi nitakuwa namkumbusha wakati huu na nitakuwa namfuatilia, amekwenda timu ambayo ina presha kidogo, kila mchezo inataka kushinda kwahiyo ajiweke tayari hata mimi presha hiyo ilinikuta nikiwa pale lakini niliziodisha juhudi sikukata tamaa.

