KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema atatumia mapumziko ya kalenda ya FIFA, kurekebisha makosa ya kikosi chake ambacho kinashika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtibwa Sugar wako mkiani mwa msimamo wakiwa na alama tano baada ya kushuka uwanjani mara tisa huku wakiwa wameshinda mchezo mmoja pekee, sare mbili na kufungwa mara tano.mtibwa sugarKatwila amesema kuwa bado kikosi chake hakijamshawishi hivyo anaanza kuwapa mazoezi maalumu wachezaji wake kabla ya kuwakabili Azam FC Novemba 24, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.

“Tuko kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu, tumeshinda mchezo mmoja pekee hivyo nafasi pekee ya kurekebisha mapungufu yetu ni kwenye kipindi hiki cha mapumziko ya kalenda ya FIFA.

“Mipango yetu sisi kama Mtibwa Sugar ni kukaa sawa tuweze kurejea kwenye ubora wetu, tunataka kuanza kupunguza makosa si jambo rahisi, nimeanza kuwaandaa wachezaji wangu ili tutakaparejea tuwe bora zaidi” amesema KatwilaJIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa