LICHA ya kukiri kuwa wanapaswa kuanza maandalizi mapema ili kufanya vizuri kwenye kundi D la Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi ameweka wazi mpango wake.

Nabi hana mpango na waarabu kabisa

Nabi amesema kuwa akili zao zote kwa sasa wamezielekeza katika kuhakikisha wanaanza vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kesho Jumamosi watakapoikaribisha Polisi Tanzania kwenye uwanja wa Mkapa Dar.

Yanga jumatatu wiki hii walishuhudia droo ya hatua ya makundi ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo kikosi chao kimepangwa kundi D pamoja na timu za US Monastir, TP Mazembe na Real Bamako.

Nabi hana mpango na waarabu kabisa

Nabi alisema: “Ni kweli tunapaswa kufanya kazi ya ziada ikiwemo kuanza maandalizi ya kikosi chetu mapema kama tunataka kufanya vizuri katika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika hasa baada ya kuwajua wapinzani wetu.

“Lakini kama timu lazima tuwe na vipaumbele na nikuweke wazi kuwa kwa sasa akili zetu zote ni katika kuhakikisha tunaanza vizuri hesabu za michezo yetu ya mzunguko wa pili kwa kushinda mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Polisi siku ya Jumamosi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa