Zanetti: Messi yuko sawa na Maradona

Beki wa zamani na timu ya taifa Argentina na klabu ya Inter Milan Javier Zanetti amesema nahodha wa timu hiyo kwasasa Lionel Messi yuko sawa na Maradona na anastahili kubeba kombe la dunia.

Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe la dunia baada ya kuifunga timu ya taifa ya Croatia kwa mabao matatu kwa bila, Huku Messi akionesha ubora mkubwa sana katika mchezo huo na kuibuka mchezaji bora wa mechi.zanettiTimu ya taifa ya Argentina itakwenda kucheza fainali ya kombe la dunia ya michuano hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa, Huku ikiwa na mtihani mkubwa wa kuisimamisha timu hiyo kubeba taji hilo kwa mara ya kwanza tangu Brazil walipofanya hivo mwaka 1962.

Gwiji Zanetti anaamini Messi yuko sawa na gwiji wa zamani wa timu hiyo Diego Armando Maradona na anaona nyota huyo anastahili kubeba taji hilo kama Maradona kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha kwenye ulimwengu wa soka.zanettiGwiji Javier Zanetti anaona Messi anastahili kabisa kubeba ubingwa wa kombe la dunia lakini pia akiwa hachukulii mchezo wa fainali dhidi ya France kua mwepesi, Kwani anaamini wana wachezaji wazuri akiwataja wachezaji kama Mbappe,Griezmann, Giroud, pamoja Adrien Rabiot.

Acha ujumbe